Siku ya wakimbizi duniani: Hali mashariki mwa DRC ikoje?
20 Juni 2022Wakiwa wanaishi ndani ya mahema yaliyokwisha kuchakaa ya angalau mita mbili na nusu, baadhi ya wakimbizi katika kambi za De la poste na Mubimbi wamekimbia ghasia za kivita kati ya makundi yenye silaha na pia kati ya jeshi la Congo na makundi yenye silaha katika vijiji vyao vya Ufamandu na Ziralo hapa kivu kusini, na wengine walitoka viviji vya Masisi, Kitchanga na Rutshuru katika mkoa jirani wa kivu ya kaskazini. Miongoni mwao wanashuhudia hali ngumu ya maisha wanayopitia kwa sasa, wakiomba kukumbukwa.UN: Mapigano ya Sahel yataongeza wakimbizi zaidi Ulaya
Narcisse Yosia ambaye ni msimamizi wa shirika la raia wa eneo la Buzi wilayani Kalehe anasema mashirika ya kiraia hapa Minova mara kadhaa yametoa mwito kwa serikali ya Congo na mashirika ya misaada ya kiutu ili kutoa huduma kwa wakimbizi hawa bila kufanikiwa.
Pamoja na vurugu zinazoendelea kuripotiwa katika mikoa jirani ya kivu ya kaskazini na Ituri, viongozi wa kiserikali wanahakikisha kwamba idadi ya wakimbizi imeongezeka, na kwamba huenda itaongezeka zaidi ikiwa vita havitakomeshwa. Hayo yameelezwa na Jospin Magambo katibu wa ofisi ya mamlaka ya serikali Minova.Wakimbizi Afrika kukabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula-UN
Jumapili, mapigano mapya yaliripotiwa kivu kaskazini kati ya jeshi la Congo FARDC na waasi wa M23 ambao hadi sasa wanadhibiti eneo la Bunagana. Mapigano yamefanyika huko Kavumba na Bikenke kati ya Runyoni na Rumangabo eneo la Bweza wilayani Rutshuru. Shirika la raia kule Rutshuru linakadiria wakimbizi zaidi ya laki moja waliokimbia vita kati ya jeshi la FARDC na M23 kule Bunagana yapata wiki moja sasa.