Sintofahamu yatanda kuhusu AFCON
17 Oktoba 2014Morocco imekanusha ripoti kuwa imejiondoa kama mwenyeji wa tamasha hilo linalozishirikisha nchi 16 lakini inataka liahirishwe kutoka tarehe za wali za Januari na Februari kwa sababu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola ambao umeyaathiri mataifa ya Afrika Magharibi.
Shirikisho la Afrika CAF limesisitiza kuwa haliwezi kuahirisha dimba hilo na kuwa litaendelea kamailivyopangwa mnamo Januari 17 hadi Februari 8.
Kama Morocco itakataa fursa hiyo basi CAF imeziomba angalai nchi mbili nyingine kama zitakuwa tayari kupewa kibali cha kuwa mwenyeji. Nchi hizo ni Ghana na Afrika Kusini. Misri pia imetajwa kama nchi inayoweza kupewa kibali.
Morocco inahofia kuwa mashabiki wengi wa kandanda na wasafiri wengine kutoka Afrika Magharibi – ambako Ebola imewauwa zaidi ya watu 4,500, inaweza kuiweka nchi hiyo ya Afrika Kaskazini katika hatari kubwa. Rais wa CAF Issa Hayatou atasafiri kwenda Morocco mwezi ujao ili kuyasikiliza malalamishi yao.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu