1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Sisi ni Charlie , lakini Sio PEGIDA"

13 Januari 2015

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo hii(13.01.2015) wamejishughulisha zaidi na suala la maandamano ya wanaopinga Uislamu maarufu kama PEGIDA na wale wanaohimiza zaidi uvumilivu na kulipinga kundi hilo la PEGIDA.

https://p.dw.com/p/1EJMa
Demonstrationen in Leipzig gegen die Pegida-Bewegung
Maandamano ya kupinga kundi la PEGIDA mjini DresdenPicha: picture-alliance/dpa

Lakini pia wahariri wameandika kuhusu mchezaji bora wa soka duniani aliyetawazwa jana mjini Zurich Uswisi.

Tukianza na gazeti la Hannoversche Allgemeine , mhariri anasema haipendezi kwa wale wanaopigania demokrasia kuugawa ulimwengu baina ya watu wazuri na wabaya na kujiridhisha kuwa uko katika upande sahihi: Mhariri anaendelea kuandika:

Na hata kwa wale wanaosimamia maadili mema hivi sasa hawana la kusema, kwasababu wengi wao licha ya kujihisi kuwa ni wananchi wanaofuata sheria , lakini msimamo wao unapingwa. Kila mmoja anatakiwa hivi sasa kuonesha kuwa anaandamana. Vipi inawezekana kufungua milango kwa wahamiaji na kusaidia ujenzi wa taifa? Ni utaratibu gani unahitajika kufanywa , ili wananchi wasifikie kuanza kuhesabu idadi ya wakimbizi waliongia nchini mwao? Na tutafanya nini kuwajumuisha vijana wa Kiislamu ambao wanaupungufu wa ujuzi wa kazi? Ni maswali matatu kati ya mengi. Tunapaswa kutafuta jibu , mhariri anasema.

Mhariri wa gazeti la Berliner Zeitung anazungumzia kuhusu jukumu la maandamano ya kundi la PEGIDA. Mhariri anasema.

Uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari kwa sasa nchini Ujerumani hauna adui mkubwa zaidi kama kundi la PEGIDA, ambapo pia vinahusika vyama vya AfD , chama mbadala kwa Ujerumani na chama cha NDP, chama kinachojulikana katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa hakiendi sambamba na haki za binadamu.

Na utoaji wa maoni na uhuru wa kupata habari sio tu nchini Ufaransa lakini pia katika bara la Ulaya haujakuwa na mtetezi madhubuti kama vikatuni vya Charlie Hebdo.

Nalo gazeti la Rhein - Zeitung linasema sisi ni Charlie lakini sio Pegida.

Ni vigumu kuelewa , kwamba kila mmoja hivi sasa anataka kutumia hofu iliyopo , baada ya kushambuliwa gazeti la Charlie Hebdo. Chama cha AfD na wafuasi wa maandamano ya PEGIDA wanayatumia mashambulio mjini Paris, kuwaonya watu kuhusu Uislamu, na kutumia hali hiyo na kuendeleza lengo lao. Ugaidi wa Waislamu wenye itikadi kali sio sawa na usambaaji wa Uislamu. Charlie Hebdo linafanya dhihaka kwa kila dini. Lakini chama cha AfD na PEGIDA wanatumia hofu iliyopo kuwa ni ugaidi na hofu juu ya Uislamu. Watu 35,000 waliojitokeza mjini Dresden wanasema "Sisi ni Charlie , lakini sio PEGIDA, hili ndio jibu sahihi kwa watu hawa.

Mhariri wa Gazeti la Neue Osnabrücker linazungumzia kuhusu kauli ya kansela Merkel kwa kundi la PEGIDA. Mhariri anasema.

Baada ya rais wa zamani wa Ujerumani Christian Wulff , sasa hata kansela Angela Merkel ametamka: Uislamu ni sehemu ya Ujerumani. Kwa sasa hilo ni muhimu kulisisitiza. Maandamano ya chuki dhidi ya Uislamu na mashambulizi ya kigaidi ya Waislamu wenye itikadi kali yanasababisha chuki zaidi na kusababisha pia mzunguko wa uadui. Ni sehemu ndogo tu ya Waislamu ambayo inatumia hatua hizi za nguvu, lakini kuwafungia nje Waislamu wote ni ujinga na inaonesha chuki tu dhidi ya watu kutoka nje.

Mada ya pili ni kuhusu kutawazwa kwa mwanasoka bora duniani hapo jana(12.01.2015) Gazeti la Dithmarscher Landszeitung limeandika:

FIFA Ballon d'Or Gala Cristiano Ronaldo Weltfußballer 2014 12.01.15
Cristiano Ronaldo mchezaji bora wa soka duniani 2014Picha: Philipp Schmidli/Getty Images

Baada ya kombe la dunia kila chombo cha habari pamoja na mitandao ya kijamii iliandika kuhusu mlinda mlango bora duniani na mchezaji bora, akiwamo Lionel Messi. Huyu alikuwa mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ujerumani Die Mannschaft , Manuel Neuer. Ni vugumu kuamini kwamba shirikisho la soka duniani limeshindwa kumtawaza Manuel Neuer kuwa mchezaji bora wa mwaka. Kwamba Messi hakufikia kuwa mchezaji bora inaeleweka kutokana na mchango wake kwa timu yake na timu ya taifa. Cristiano Ronaldo ama Neuer wamefanya vizuri , Neuer katika timu ya taifa na Cristiano katika klabu yake hili halina ubishi. Pamoja na shaka yoyote ile tunapaswa kuheshimu ushindi wa mshambuliaji huyo raia wa Ureno na kumpongeza.

Na pia hongera zimwendee kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew kwa kustahili kupata taji la kocha bora.

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman