1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yachaguliwa kuwa mwanachama baraza la usalama UN

7 Juni 2024

Denmark, Ugiriki, Pakistan, Panama na Somalia zimechaguliwa kuwa wanachama wasio wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka Ujao wa 2025.

https://p.dw.com/p/4gmYd
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika vikao vyake
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika vikao vyakePicha: Loey Felipe/UN Photo/Xinhua/picture alliance

Baraza kuu la Umoja huo wa Mataifa lilizichagua nchi hizo tano jana alhamisi,kuchukuwa nafasi zinazoshikiliwa hivi sasa na Ecuador, Japan, Malta, Msumbiji na Uswisi. 

Baraza la Usalama ndio chombo pekee cha Umoja wa Mataifa chenye mamlaka ya kupitisha maazimio yanayolazimika kutekelezwa kwa mujibu wa  sheria ya Kimataifa. 

Soma pia:Watu mil 114 wakimbia makazi yao kutokana na vita duniani

Baraza kuu la Umoja wa mataifa pia limemchaguwa waziri mkuu wa zamani wa Cameroon,Philemon Yang,kuwa  rais mpya asiye na mamlaka makubwa  atakayeiongoza taasisi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW