1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yapiga marufuku mifuko ya plastiki

Josephat Charo
2 Oktoba 2024

Somalia imeweka marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki iliyocheleweshwa kwa muda mrefu kusaidia kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.

https://p.dw.com/p/4lKDY
takataka za plastiki
Takataka zikiwa na rundo la mifuko ya plastiki.Picha: Yuyun Ismawati/2024

Sheria hiyo mpya iliyotangazwa kwa mara ya kwanza mnamo Februari 2024 inazuia uagizaji kutoka nje, utengenezaji, uuzaji na utumiaji wa mifuko ya plastiki ambayo huishia kutupwa kama taka au kuzikwa ardhini.

Wanaharakati wa mazingira na wakaazi wa mji mkuu Mogadishu wameipongeza marufuku hiyo wakisema ilichelewa.

Soma zaidi: Somalia yasema vitendo vya Ethiopia vinakiuka uadilifu wake

Somalia inajiunga na nchi nyingine za Afrika, zikiwamo Kenya na Tanzania, ambazo zilipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.

Marufuku ya Somalia inaanza kutekelezwa baada ya wajumbe kukamilisha mkutano mjini Nairobi siku ya Jumatatu (Septemba 30) wakiwa na matumaini ya kufikia mkataba wa kwanza wa kimataifa kuhusu uchaguzi unaosababishwa na plastiki.