1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yasaini mkataba wa kijeshi kuimarisha usalama

12 Mei 2017

Somalia imesaini kile kilichoitwa "mkataba wa utulivu" na jumuiya ya kimataifa wenye lengo la kurejesha hali ya usalama, kuimarisha jeshi lake, kukabiliana na njaa pamoja na kufufua uchumi wake uliodorora.

https://p.dw.com/p/2cr0l
Großbritannien Somalia-Konferenz
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Hill

Baada ya kusainiwa mkataba huo kati ya Somalia na mtandao wa kimataifa wa  wenye kushiriki jitihada za kulisadia taifa hilo, Rais Mohammed Abdullahi Mohamed amesema katika mkutano wa mjini London, Uingereza, kwamba siku ya kusaini mkataba huo ni ya kihistoria kwa Somalia.  Kiongozi huyo ambae anafahamika kwa jina la utani Famajo aliendelea kusema zama mpya kwa taifa la Somalia zimepata unafuu mkuibwa.  Matarajio kwa raia wa taifa hilo ni makubwa sana na kwamba utekelezaji wake sio suala la mjadala.

Somalia na mataifa 17 washirika wake wamehifadhi makubaliano ya kurasa 17 yakijikita katika suala la usalama. Makabuliano hayo yanaweka matumaini ya uwepo wa misingi ya amani na mafanikio katika taifa hilo lililovurugika kabisa barani Afrika.

Matumani mapya Somalia

Somalien Armee
Wanajeshi wa Somalia wakiwa katika mafunzoPicha: Getty Images/AFP/P. Moore

Baada ya zaidi ya miaka 20 ya mgogoro usiokiwisha, uliosababisha machungu na hali ngumu, kumeibuliwa aina zote za fursa ambazo litafanikisha taifa hilo kuwa hadithi mpya ya mafanikio.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye alikuwa miongoni mwa wenyeji wa hafla hiyo, amesema Somalia itakuwa na mafanikio. Mkataba huo una lengo la kufanya kazi ya kuipatia msamaha wa madeni Somalia na kuisaidia kupambana na wapiganaji wa kundi la mitazamo mikali ya Kiislam al-Shabaab, ambalo kwa muongo uliopita limekuwa likijaribu kuipindua serikali ya Somalia.

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa aliongeza kusema taifa hilo kwa sasa ina serikali ambayo inaweza kuaminika na mipango ambayo inaonesha matumaini. Lakini pamoja na kutolewa kwa mchango wa euro milioni 550 kama msaada kwa ajili ya kukabiliana na ukame, ameonya kuwa kiasi kingine cha euro milioni 900 kwa sasa kuhitajika katika miezi kadhaa ijayo ili kudhibiti hali mbaya inayoongozeka kutumbukia katika balaa la njaa.

Watu milioni sita wakabiliwa na njaa

Raia milioni sita wanakabliwa na njaa milioni sita, kiasi ambacho kinakaribia kuwa nusu ya idadi jumla ya wakazi wa taifa hilo, kwa hivi sasa wanategemea msaada wa chakula cha dharula. Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Peter de Clercq aliwaambia waandishi habari kuwa kushindwa kunyeshwa kwa misimu miwili ya mvua kumesababisha watu kuishi katika mazingira magumu kabisa.

Anasema watu wamekuwa wakikimbilia maeneo ya mijini ili kuweza kujitafutia chakula. Hali imeendelea kuwa mbaya zaidi. Na kwamba kama hakutakuwa na jitihada madhubuti hadi mwishoni mwa mwaka taifa hilo litaingia kwa ukamilifu katika balaa la njaa. Juma lililopita Umoja wa Mataifa ulisema Somalia itakuwa na watoto milioni 1.4 wenye utapiamlo sugu ifikapo mwishoni mwa mwakla ikiwa asilimia 50 zaidi ya mwaka 2016.

Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Boris Johnson, akiwa waandalizi wenza wa mkutano huo Farmajo na Guterres wamesma watakuwa na namna ya kuiepusha Somalia majanga kama wadau wote watajumisha nguvu zao kwa pamoja.

Mwandishi: Sudi Mnette/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef