1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stoltenberg aitaka Marekani iendelee kushirikiana na Ulaya

4 Aprili 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg, ameihimiza Marekani iendelee kushikamana na Ulaya wakati muungano huo wa kijeshi ukiadhimisha miaka 75 tangu ilipoasisiwa.

https://p.dw.com/p/4ePtk
Mkutano wa NATO
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg (katikati), akiwa kwenye gwaride la muungano huo wa kijeshi mjini Brussels, Ubelgiji, tarehe 4 Aprili 2024.Picha: Kenzo Tribouillard/AFP

Stoltenberg amesema haamini kuwa Marekani wala Ulaya ziinaweza kuishi kwa kutengana, bali anaamini kuwa pande hizo mbili zinapaswa kushirikiana kwa pamoja ndani ya NATO, kwa sababu kimsingi zinakuwa imara zaidi na salama pamoja.

Stoltenberg amesisitiza kwamba Amerika Kaskazini inaihitaji Ulaya na kupitia Ulaya, Marekani ina marafiki na washirika wengi zaidi kuliko dola lolote jengine kubwa.

Soma zaidi: Mawaziri kuadhimisha miaka 75 ya kuundwa kwa Jumuiya ya NATO

Maadhimisho ya leo yamegubikwa na vita vya Urusi nchini Ukraine na uwezekano wa Donald Trump kurejea madarakani kama rais wa Marekani.

Stoltenberg amependekeza msaada wa euro bilioni 100 katika kipindi cha miaka mitano kuisaidia Ukraine.