1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan Kusini yasaini mkataba wa amani na wanamgambo

OMAR MUTASA31 Agosti 2020

Kiongozi wa serikali ya mpito ya Sudan Kusini Abdul Fatah Burhan amesaini mkataba wa amani na vyama vya wapiganaji wa Sudan kuhusu kugawana madaraka na pia wakimbizi walioko nje ya Sudan waweze kurejea nyumbani. 

https://p.dw.com/p/3howh
Südsudan Juba Unterzeichnung Friedensvertrag mit Rebellen
Picha: Reuters/S. Bol

Hatimae haiwi haiwi imekuwa rais Salva Kiir amezitaka pande zote zihishimu mkataba huu ambao umevileta pamoja karibu vyama kumi vya wapiganaji vingi ya vyama hivyo vikiwa kutokea jimbo la Darfur. Bw Jibril Ibrahim kiongozi wa chama cha Justice and Equality Movement amezungumza kwa niaba ya makundi ya wapiganaji wa jimbo la Darfur Je sasa watu wa Darfur wataweza kushirikishwa kwenye serikali hii

"Nadhani tumesaini mkataba mzuri na tutakuwa ndani ya serikali kuweza kutoa maamuzi yakutekeleza mkataba huu,"Jibril amesema.

Nae Malik Aggar kiongozi wa chama cha SPLM/North ambacho kimekua kikipiga vita serikali ya Sudan kwa muda wa miaka 30 nimemuuliza kwanini kila mara amekua akitoa hutuba yake huku akimtizama Gen Burhan Abdulfatah kiongozi wa Sudan

"Ujumbe umekuwa tunataka mkataba huu utekelezwe kwa moyo wa dhati kwa maana mikataba ya kwanza imekuwa ikikosa kuheshimiwa," amesema Malik Aggar.

Mkataba huo wa amani umesainiwa kati ya serikali ya Sudan Kusini na makundi matano ya wapiganaji
Mkataba huo wa amani umesainiwa kati ya serikali ya Sudan Kusini na makundi matano ya wapiganajiPicha: Reuters/S. Bol

Malik amesema wanataka sasa jeshi liwe moja na idara ya usalama iwe moja huku akisisitiza kuwa lazima mlio wa mtutu wa Bunduki usimamishwe .

Kiongozi wa chama cha Sudan Revolutionary front Alhadi Idris Yahya amemsifu rais Yoweri M7 kwa msaada wake. 

Ameendelea kusema: "Ndiyo. Rais Museveni na watu wa Uganda wamo kwenye moyo wetu pamoja na watu wa Eritrea wametusaidia sana wakati wa mapambano na ambapo mataifa mengi yalikataa kutusaidia."

Bw ALHADI IDRISS amekubaliana na hutuba ya rais Salva Kiir kuwa mkataba huu bado haujakamilika kundi la Sudan Liberation Mov na kundi njengine la SPLM /North Wamejiondoa kwenye mkataba huu . Na sasa mkuu wa UNAMID amesema shetani mkubwa aliebakia ni kutekeleza mkataba huu .