Sudan Kusini yasitisha huduma za mitandao ya kijamii
23 Januari 2025Mkurugenzi Mkuu wa Kitaifa wa Mamlaka ya Mawasiliano Napolepon Adok, amesema kwenye barua kwa watoa huduma hizo kwamba, hatua hiyo ilitarajiwa kuanza kutekelezwa usiku wa Jumatano.
Adok amesema haya yanatokana na machafuko ya hivi karubuni nchini humo, ambayo yamewaweka wakaazi wa Sudan Kusini kwenye viwango vya ukatili wa hali ya juu kupitia maudhui ya mitandao ya kijamii.
Soma pia: Rais Kiir awatimua gavana, wakuu wa jeshi na polisi
Watumiaji wanaopata huduma kupitia kampuni ya MTN nchini Sudan Kusini na mtandao wa Zain hawataweza kupata huduma Facebook, TikTok na mitandao mingine kwa hadi siku 90, yamesema makampuni hayo kwenye taarifa jana Jumatano.
Karibu raia 16 wa Sudan waliuawa wiki iliyopita wakati ghasia zilizuka katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba na kwingineko nchini humo.