Sudan yaadhimisha mwaka mmoja wa mapinduzi dhidi ya Bashir
11 Aprili 2020Mwaka mmoja uliopita , mamia kwa maelfu ya raia wa Sudan walifanya maandamano ya wiki nzima mbele ya makao makuu ya jeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
Mwanafunzi kijana mwanamke , Alla Salah , alisimama juu ya kipaa cha gari akiimba kauli mbiu za kisiasa, baadaye alikuja kuwa ishara ya vuguvugu la maandamano katika jamii ambayo kwa kiasi kikubwa inadhibitiwa na wanaume zaidi.
Kila mmoja aliingia mitaani, ikiwa ni pamoja na maprofesa, waalimu na madaktari. Wasanii waliandika ujumbe na kuchora picha za uhuru katika kuta mjini Khartoum.
Kwa miezi kadhaa , nchi hiyo ilikuwa ikitokota hadi hatimaye kile ambacho hakikufikirika kikatokea: dikteta Omar al-Bashir alipinduliwa Aprili 11, 2019, baada ya karibu miongo mitatu madarakani.
Yalikuwa mapinduzi yaliyoelezwa na wengi kuwa ni vuguvugu la mapinduzi ya mataifa ya Kiarabu namba mbili. Raia walijisikia furaha kubwa.
Lakini mwaka mmoja baadaye, katika kusherehekea mwaka mmoja wa siku hii kubwa, hali mjini Khartoum imenyong'onyea.
Kwasababu ya janga la virusi vya corona, shule na vyuo vikuu vimefungwa. Sherehe za maadhimisho , kupeperusha bendera na kuimba wimbo wa taifa ama nyimbo za mapinduzi, vimefanyika nyumbani ama katika mitandao ya kijamii.
Lakini kuna sababu nyingine ya hali hiyo ya kunyong'onyea: Baada ya miezi 12 ya uhuru wa kisiasa , Sudan haijapiga hatua ambayo ilipigiwa matumaini.
Nchi hiyo iko imara kisiasa lakini tete. Uchumi wake umeporomoka kabisa, na janga la virusi vya corona , linatishia kuharibu mafanikio madogo nchi hiyo iliyoyapata katika miezi 12 iliyopita katika kufufua biashara na uchumi.
Sudan ni mshirika mdau muhimu katika eneo la kanda hiyo. Ni nchi ya tatu kwa mkubwa katika bara la Afrika , pamoja na watu wake milioni 42 inaonekana kuwa ni daraja kati ya Afrika na ulimwengu wa Kiarabu. Sudan pia ni moja kati ya nchi muhimu za kupitia watu wanaokwenda kusaka uhamiaji kutoka bara la Afrika.
Iwapo hali ya kisiasa na kiuchumi itakuwa bora , Sudan inaweza kutoa fursa ya uwekezaji kutoka nje, kwa mfano katika sekta ya mafuta na kilimo.
Lakini kwa hivi sasa , Sudan imelala, na kutishia kuleta madhara makubwa kutokana na hali hiyo kwa eneo la kanda hiyo, anasema Philipp Jahn , mkuu wa kituo cha utafiti wa wakfu wa Friedrich Ebert nchini Sudan.
Licha ya mabadiliko chanya ya kisiasa , Sudan haikuweza