Sudan yaipongeza hatua ya Pompeo
3 Agosti 2020Matangazo
Vyombo vya habari nchini Sudan vinasema serikali nchini humo imefurahishwa na matamshi ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kwamba anataka kuiondoa Sudan kutoka kwenye orodha ya wafadhili wa ugaidi.
Pompeo ametoa kauli hiyo mara kadhaa kwani kuiweka Sudan kwenye orodha hiyo ni jambo linalozuia uwekezaji katika nchi hiyo. Lakini kuna kutoelewana kuhusiana na kiwango cha fidia itakayotolewa kutokana na mashambulizi ya mabomu ya balozi mbili za Marekani.
Pompeo ameiambia kamati ya mambo ya nje ya baraza la seneti la Marekani kuwa maelewano yatafikiwa hivi karibuni na kuwasilishwa mbele ya bunge. Serikali ya Sudan kwa upande wake imesema itachukua hatua zote ili kutimiza vigezo vya Marekani vitakavyosaidia maamuzi kwenda upande wao.