Sweden kutojadiliana na Hungary kuhusu NATO
26 Januari 2024Matangazo
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ameeleza imani yake kuwa bunge la Hungary litaidhinisha ombi la Sweden mwishoni mwa mwezi huu.
Mawaziri wakuu wa Sweden na Hungary watakutana wiki ijayo mjini Brussels, lakini Kristersson amesema Sweden haitatoa ahadi zozote mpya kuhusu NATO wakati wa mkutano huo.
Soma zaidi: Bunge la Uturuki laidhinisha Sweden kujiunga na NATO
Sweden na Finland zilituma maombi ya kujiunga na jumuiya hiyo ya kujihami mwaka 2022 baada ya Urusi kuivamia Ukraine.
Hata hivyo, uwanachama wao ulipingwa na Uturuki na Hungary na kuziacha nchi hizo katika njia panda.
Washirika wa NATO wanaiona Sweden kama kiungo muhimu katika usalama eneo la Baltiki.