1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden yataka mwandishi anaeshikiliwa kwa miaka 20 kuachiwa

23 Septemba 2021

Waziri Mkuu wa Sweden ameitolewa wito Eritrea kumuachia huru mwandishi habari wa Sweden mwenye asili ya Eritrea, ambaye anashikiliwa bila mshtaka kwa miongo miwili sasa.

https://p.dw.com/p/40im4
Dawit Isaak
Picha: Kalle Ahlsén

Wito huo umetolewa wakati Shirika la Waandishi Wasio na Mipaka, RSF, likiziomba mamlaka nchini Sweden kuchunguza ukiukaji wa haki za binaadamu katika kesi hiyo.

Mwandishi huyoa Dawit Isaak, alikuwa miongoni mwa kundi la watu zaidi ya 20, wakiwemo mawaziri, wabunge na waandishi habari huru waliokamatwa nchini Eritrea mwezi Septemba 2001.

Waziri Mkuu wa Sweden Stefan Lovfen, amesema katika ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba muda aliowekwa kizuwizini Isaak ni mrefu sana.

Amesema serikali yake na serikali zilizopita zimeshughulikia pakubwa kesi ya Dawit, na kuongeza kuwa ingawa kazi yao haijazaa matunda mpaka sasa, lakini hawatakata tamaa.

Shirika la RSF limerejelea wito wake kwa waendesha mashtaka wa Sweden kuchunguza uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika kesi hiyo.

Sheria ya Sweden iliyopitishwa mwaka 2014, inawezesha kushtakiwa kwa uhalifu kama huo, hata kama umetendeka kwingineko duniani.