1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUswidi

Sweden yatwaa mshindi wa tatu Kombe la dunia la wanawake

Sylvia Mwehozi
19 Agosti 2023

Sweden imeharibu tafrija ya mwenyeji mwenza wa mashindano ya Kombe la dunia la wanawake Australia baada ya kutwaa nafasi ya tatu kwa ushindi wa mabao 2-0 mjini Brisbane.

https://p.dw.com/p/4VM2N
Kombe la dunia la wanawake
Wachezaji wa timu ya Sweden wakishangiliaPicha: Darren England/AAP/IMAGO

Sweden imeharibu tafrija ya mwenyeji mwenza wa mashindano ya Kombe la dunia la wanawake Australia baada ya kutwaa nafasi ya tatu kwa ushindi wa mabao 2-0 mjini Brisbane. Sweden ilichapwa na Uhispania katika nusu fainali ya Jumatano. 

Mbele ya umati wa karibu watazamaji 50,000, Sweden walijiweka mbele baada ya kufunga bao la mkwaju wa penalti katika dakika ya 30 uliopigwa na Fridolina Rolfo na kuongeza bao kali la pili kutoka kwake Kosovare Asllani kipindi cha pili. Hii ni mara ya nne kwa Sweden kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo.

Michuano ya mwaka huu iliyoandaliwa na New Zealand kwa kushirikiana na Australia, inatajwa kuwa bora zaidi kuwahi kutokea.

Kilele cha michuano hiyo kitakuwa kesho katika fainali itakayo zikutanisha timu za England na Uhispania mjini Sydney.