1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"EU haikuwa wazi kuhusu muafaka wa uhamiaji na Tunisia"

23 Oktoba 2024

Taasisi ya uangalizi wa maadili ya Umoja wa Ulaya imesema umoja huo haujawa wazi kikamilifu kuhusu hatari za haki za binaadamu zinazohusiana na mkataba wa uhamiaji na Tunisia uliogubikwa na madai ya unyanyasaji.

https://p.dw.com/p/4m9Nm
Tunisia | Kushughulika na wahamiaji
Wahamiaji wa Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaojaribu kuvuka kuelekea Italia walipozuiliwa nchini Tunisia. Juni 9, 2023Picha: Hasan Mrad/ZUMA Wire/IMAGO

Chini ya makubaliano ya mwaka wa 2023, kundi hilo lenye nchi 27 wanachama limetoa fedha kwa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ili nayo isaidie katika kudhibiti uhamiaji wa kutumia boti ndogo ndogo kuingia Ulaya. Sheria za ufadhili za Umoja wa UIaya zinasema fedha zote zinapaswa kutumiwa katika njia inayoheshimu haki za msingi, lakini ripoti zimeibuka za wahamiaji wakichapwa, kubakwa na kunyanyaswa na maafisa wa Tunisia. Taasisi hiyo ya Umoja wa Ulaya imesema leo kuwa Halmashauri Kuu ya Ulaya haikuweka hadharani ripoti ya tathmini ya hatari iliyofanywa kabla ya makubaliano hayo kutiwa saini, na haikueleza waziwazi ni chini ya mazingira gani fedha hizo zingesimamishwa.