Idara ya utabiri wa hali ya hewa Kenya imeitaka serikali kujiandaa kwa mvua kubwa ya El Nino inayotarajiwa wakati wowote kutoka sasa hadi mwezi Disemba, huku ikitoa tahadhari ya mafuriko na mmomonyoko katika maeneo ya pwani, magharibi na Bonde la Ufa nchini humo. Serikali ya Kenya inakadiria kwamba inahitaji shilingi bilioni 10 kukabiliana na athari za mvua ya El nino. Msikilize wakio Mbogho.