Takriban raia 11 wameuawa mashariki mwa DR Congo
25 Machi 2024Mamlaka kwenye eneo hilo imelilaumu kundi la waasi la ADF kwa mashambulizi hayo. Augustin Kapupa, afisa katika eneo la Matembo lililokumbwa na shambulio mojawapo amesema watu sita waliuawa kwenye shambulio la Jumamosi usiku.
Kwa mujibu wa afisa wa serikali mjini Beni Makofi Bukuku mj wa Sayo ni eneo la pili lililoshambuliwa ambako watu watano waliuawa.
Mwanahabari mashuhuri wa DRC ahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela
Ameliambia shirika la habari la AFP kwamba idadi ya waliouawa katika mji huo wa Sayo bado inaweza kuongezeka, huku waasi wakiwa bado wapo katika eneo hilo.
Jumuiya ya kiraia ya Matembo, imesema wakazi wa eneo hilo katika muda wa wiki tatu zilizopita wamekuwa wakielezea wasiwasi wao kwa jeshi kutokana na kuwepo kwa waasi katika eneo hilo.