1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Taliban washiriki mkutano wa faragha na Umoja wa Mataifa

1 Julai 2024

Mkutano wa siku mbili wa Umoja wa Mataifa unaojadili masuala ya Afghanistan unaendelea mjini Doha ukiwaleta pamoja wawakilishi kutoka mataifa 30 pamoja na mashirika ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/4hj4a
Qatar | Taliban-Mkutano mjini Doha
Doha mji mkuu wa Qatar ni mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya mambo nchini Afghanistan ambapo ujumbe wa Taliban unaoongozwa na Zabihullah Mujahid utakutana na wawakilishi wa nchi mbalimbali.Picha: Zabihullah Mujahid

Mkutano wa siku mbili wa Umoja wa Mataifa unaojadili masuala ya Afghanistan unaendelea mjini Doha ukiwaleta pamoja wawakilishi kutoka mataifa 30 pamoja na mashirika ya kimataifa.

Ujumbe wa Taliban unaoongozwa na msemaji wa serikali Zabihullah Mujahid unashiriki mazungumzo hayo ya faragha yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa.

Soma pia: Taliban: Haki za wanawake wa Afghanistan ni suala la ndani

Pembezoni mwa mkutano huo Taliban imefanya mazungumzo pia na wawakilishi wa mataifa kama Urusi, India na Saudi Arabia kabla ya mkutano rasmi kuanza hapo jana nchini Qatar.

Ushiriki wa Taliban unaashiria mabadiliko kutoka Februari ambapo walikataa kuhudhuria mkutano kama huo.

Umoja wa Mataifa unajaribu kusukuma ajenda mbalimbali ikiwemo haki za binadamu, haki za wanawake, na ujumuishaji katika kisiasa, lakini Taliban bado wanahofia ushawishi wa nje.