1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taliban yakanusha madai ya Pakistan kushambulizi mipakani

12 Septemba 2023

Kundi la Taliban limepinga shutma za serikali ya Pakistan kwamba, ndilo la kulaumiwa kwa kufungwa kwa mpaka muhimu kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4WFrU
Wanajeshi wa Taliban wakiwa katika majukumu yao
Wanajeshi wa Taliban wakiwa katika majukumu yaoPicha: Zerah Oriane/Abaca/picture alliance

Pakistan iliufunga mpaka wa Torkham upande wa kaskazini magharibi Jumatano iliyopita baada ya walinzi wa nchi hizo mbili kushambuliana kwa risasi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Pakistan Mumtaz Zahra Baloch ameushtumu utawala wa Talibankwa kujenga majengo haramu kwenye maeneo ya mipaka na kufanya mashambulizi ya risasi kama uchokozi. 

Soma pia:Taliban yasaini makubaliano yenye thamani ya dola bilioni 6.5 nchini Afghanistan

Baloch amerudia madai kwamba Afghanistan inaruhusu ardhi yake kutumika na wanamgambo kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistan.

Matamshi ya Baloch yameukasirisha utawala wa Taliban, huku afisa mmoja wa Taliban akiitaja serikali ya Pakistan kama "isiyokuwa na uwezo" na kwamba haiwezi kuhakikisha usalama wa taifa.

Nchi hizo mbili, Afghanistan na Pakistan, zimekuwa zikilaumiana kwa muda mrefu juu ya mzozo kwenye mipaka yao na suala la usalama.