1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuandaa kumbukumbu ya walioangamia Magdeburg

24 Desemba 2024

Mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Magdeburg unatarajiwa kuandaa tamasha la kuwakumbuka waathiriwa wa shambulio katika soko la Krismasi lililotokea mjini humo Ijumaa ya tarehe 20 Desemba.

https://p.dw.com/p/4oYRz
Magdeburg
Tamasha la kuwakumbuka walioangamia Magdeburg kufanyika Alhamisi Picha: AFP

Tukio hilo lilisababisha mauaji ya watu watano akiwemo mtoto wa miaka 9, huku watu wengine zaidi ya 200 wakijeruhiwa. 

Tamasha hilo litafanyika katika soko jengine la krismasi katika eneo la kati ya mji huo. Serikali ya jimbo hilo imesema itatoa tiketi 200 za bure kwa waathiriwa, familia zao na kwa watoa huduma za dharura baada ya kujadiliana na meya wa mji huo. 

Idadi ya waliojeruhiwa kwenye mkasa wa Magdeburg yaongezaka

Tamasha hilo litaanza kwa watu kunyamaa kwa dakika moja kuwakumbuka walioangamia katika mkasa huo, baada ya mwanamume mmoja wa miaka 50 mwenye asili ya kiarabu aliye pewa jina la Talib A, kuvurumisha gari lake katika soko hilo na kusababisha mauaji ya watu watano. Kwa sasa anaendelea kuzuiliwa na polisi.