1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania na Burundi zasaini makubaliano ya ujenzi wa reli

17 Januari 2022

Tanzania na Burundi zimesaini makubaliano ya ujenzi wa reli yenye thamani ya dola milioni 900.

https://p.dw.com/p/45dFi
Tansania Zugfahren in Dar es salaam
Picha: Ericky Boniphace

Reli hiyo itayaunganisha mataifa hayo mawili, na wanatafuta wafadhili wa kifedha kwa ajili ya mradi huo, kwa mujibu wa wizara ya fedha ya Tanzania.

Reli hiyo yenye urefu wa kilomita 282, inayounganisha mji wa magharibi mwa Tanzania wa Uvinza na mji mkuu wa kisiasa wa Burundi, Gitega, ndiyo hatua ya karibuni zaidi kuelekea lengo la Tanzania la kujenga mtandao wa reli wa kilomita 2,561, kuimarisha biashara ya kanda.

Mizigo yenye uzito wa zaidi ya tani milioni moja itasafirishwa kupitia reli kati ya mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki, na itasafirisha pia tani milioni tatu za madini kutoka Burundi kwenda Tanzania kila mwaka.

Taarifa hiyo ya wizara ya fedha ya Tanzania imeongeza kuwa mataifa hayo yanatafuta ufadhili wa mradi huo, unaonuwiwa kupunguza gharama za usafirishaji, kuharakisha maendeleo ya viwanda na kuboresha uchumi jumla wa kanda.