Vyombo vya habari
Tanzania: Nipashe Jumapili lajifungia lenyewe
16 Januari 2018Matangazo
Ni katika kile kilichosemekana kama kuenzi uwajibikaji baada ya kuchapisha habari iliyohusu rais Magufuli kutaka watu wasiendeleze mjadala kuhusu ukomo wa urais na kuufananisha na utawala wa rais Paul Kagame wa Rwanda ni jambo linaloendelea kuzua gumzo nchini Tanzania.
Gazeti la Nipashe Jumapili limejifungia kwa miezi mitatu pamoja na kumuomba radhi Rais Mafufuli na Rais Kagame. Lakini baadhi ya wadadisi wanahisi hatua hiyo ya gazeti la Nipashe haikustahili. Kwa mengi zaidi DW imezungumza na mwandishi mkongwe katika tasnia hii ya uandishi habari Salim Salim aliyeko nchini Tanzania na kwanza anatoa maoni yake juu ya hatua hiyo.