Tanzania yaidhinisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda
21 Februari 2023Matangazo
Bomba hilo litakalokuwa na urefu wa zaidi ya kilometa 1,400 litasafirisha mafuta ghafi kutoka kwenye visima vinavyoendelezwa eneo la ziwa Albert kaskazini magharibi mwa Uganda hadi kwenye bahari ya Hindi upande wa Tanzania
Ujenzi wake ulihitaji idhini kutoka mataifa yote mawili na mwezi uliopita Uganda tayari ilitoa kibali cha mradi huo kwa kampuni itakayoendesha bomba hilo ya East African Crude Oil Pipeline.
Mkuu wa kampuni hiyo nchini Tanzania amesema kutolewa kwa kibali cha Tanzania hii leo kunafungua milango ya kuanza kwa ujenzi wa mradi huo ambao makundi watetezi wa haki za binadamu na mazingira wanaupinga kwa madai kwamba utaharibu makaazi ya watu na ikolojia.