Rais wa Kenya William Ruto amesema tatizo la kucheleweshwa mishahara ya wafanyakazi wa umma limepatiwa ufumbuzi. Awali Waziri wa fedha Njuguna Ndung'u alikuwa amewataka wafanyakazi hao kujifunga mkanda, kwa hoja kuwa serikali inakabiliwa na mseto wa changamoto katika ukusanyaji kodi, na ugumu wa kupata mikopo mipya.