Taytu Betul, anaetajwa kuwa ni mmoja wa viongozi shupavu wa Ethiopia, alikuwa ni mke wa mfalme Menelik wa Pili. Malkia huyo alichangia pakubwa katika kuvishinda vikosi vya Italia, ilipojaribu kuitawala Ethiopia, na ndiye aliyetoa jina la mji mkuu wa Addis Ababa.