1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran iko tayari kwa ushirikiano au mapambano

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHO

Nchi ya Iran inaonya kuwa iko tayari kwa ushirikiano au mapambano kuhusiana na suala la mpango wake wa nuklia na vikwazo ilivyowekewa.Hii inatokea baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa linawekea nchi hiyo vikwazo vipya baada ya kukataa zaidi ya mara moja kusitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium ambao unaweza kutumiwa kutenheza silaha za nuklia.

Kwa mujibu wa naibu waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Abbas Araghchi nchi yake iko tayari kushirikiana na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa au kupambana na vikwazo vikali itakavyowekewa.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa linakutana wiki hii kuidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Iran baada ya kukataa kusitisha mpango wa kurutubisha madini ya uranium.

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad anasema atashiriki katika mkutano wa baraza hilo ili kutetea haki ya nchi yake kuwa na mpango wa nuklia japo awali alieleza baraza hilo kutokuwa halali.Mataifa ya magharibi kwa upande wake yanahofia kwamba Iran huenda ikatengeza silaha za nuklia katika mpango huo wa kutengeza nishati ya nuklia jambo inalokanusha.