1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Teknolojia yazusha utata Kombe la Mabara

19 Juni 2017

Michuano ya Kombe la FIFA la Mabara inaendelea Urusi, lakini maamuzi yanayotokana na teknolojia ya video hayalipi Shirikisho hilo la kandanda duniani suluhulisho la haraka katika dimba hilo

https://p.dw.com/p/2exDF
Russland Confed-Cup Kamerun - Chile
Picha: picture-alliance/Offside/S. Stacpoole

Mechi zote mbili zilizochezwa jana Jumapili ziliziacha timu zikiwa zimechanganyikiwa kutokana na maamuzi yaliyofanywa na marefa walioshauriana na merefa wasiadizi waliokuwa watazama picha za video zinazorudiwa mara kadhaa. Mabao ya Ureno na Chile yalikataliwa kwa sababu yalikuwa ya kuotea. Ureno ililazimika kusubirikwa kile kilichoonekana kuwa ni tathmini ya video ambayo haikuhitajika kuamua kuhusu bao safi sana lililokuwa limefungwa. Mskilize kocha wa Chile JUAN ANTONIO Pizzi "nadhani mfumo huu unahitaji muda. Tunaufanyia majaribio sasa. Hivyo kama ni kweli kuwa baadhi ya hisia huenda labda zikachanganya kwa sababu tumezoea hali tofauti katika ulimwengu wa kandanda. Tunapaswa kusubiri na kuona itakavyokuwa

Fußball Testspiel Schiedsrichter FIFA
Mfumo wa video unafanyiwa majaribioPicha: picture-alliance/Pressefoto Ulmer/M. Ulmer

HUGO BROOS, kocha wa Cameroon pia alizungumzia teknolojia hiyo "Nadhani imedhihirisha mara mbili kuwa inaweza kuwa muhimu sana kama goli lililofungwa tu kabla ya kipindi cha pili ambalo lilikuwa la kuotea. Kwa maana hiyo inasaidia sana. Ukweli upo. Lilikuwa la kuotea na likafutwa. Lakini kama tutaendelea kufanya hivyo mara kadhaa kwenye mchezo na uamuzi kuchukua muda fulani, haiwafurahishi sana wachezaji. Mchuano wa Ureno na Mexico ulikamilika kwa sare ya 2-2, wakati Chile ikiilaza Cameroon 2-0.

Mfumo wa video huenda una mambo mengi ya kulidhihirishia jopo linalotunga sheria za kandanda – IFAB. Uamuzi unapaswa kutolewa mwezi Machi kama matumizi ya teknolojia ya video yataidhinishwa katika Kombe la Dunia au la.

Matukio manne katika siku ya pili pekee ya dimba hilo kubwa mpaka sasa kufanyiwa majaribio ya moja kwa moja yamezusha utata kuliko FIFA ilivyotarajia.

mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Josephat Charo