1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Wabunge wa Israil kuamua iwapo Rais Moshe Katsav anapaswa kujiuzulu au la.

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXy
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Beranard Kouchner.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Beranard Kouchner.Picha: AP

Wabunge wa Israil wanatarajiwa kuamua iwapo Rais Moshe Katsav aondoke au asiondoke madarakani hata baada ya shinikizo kuongezeka kumtaka rais huyo ajiuzulu.

Rais Moshe Katsav amekanusha vikali madai ya ubakaji na bughdha ya kijinsia yaliyotolewa dhidi yake.

Rais huyo alisema atajiondoa kwa muda kutoka wadhifa huo usiokuwa na uzito wa utendaji lakini hatajiuzulu.

Iwapo bunge litakataa ombi la Rais Moshe Katsav ajiondoe kwa muda, rais huyo ataendelea kubaki madarakani na hivyo kuzidisha shinikizo zinazomtaka ajiuzulu au bunge limuuzulu madaraka yake.

Waziri Mkuu wa Israil, Ehud Olmert, amesema kwa hali ilivyo, Rais Moshe Katsav hana budi ila ang´atuke.

Kura ya maoni inaonyesha raia wengi wa Israil wanamtaka Rais huyo kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo.