1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv yamtangaza Guterres mtu asiyetakiwa Israel

2 Oktoba 2024

Israel imemtangaza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwa mtu asiyetakiwa kuonekana nchini humo kwa madai ya kushindwa kuyalaani vikali mashambulizi ya makombora la Iran dhidi ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4lLDw
Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ambaye Israel imemtangaza mtu asiyetakiwa kuonekana nchini humo kwa madai ya kutolaani vikali mashambulizi ya Iran dhidi ya Tel Aviv.Picha: William Volcov/ZUMA Press Wire/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz, amesema hatua ya Guterres kushindwa kuilaani Iran inamfanya kuwa mtu asiyetakiwa ndani ya Israel.

Katz aidha amesema sio tu mtu, hata nchi yoyote ulimwenguni itakayoshindwa kufanya hivyo haipaswi kukanyaga ardhi ya Israel.

Soma zaidi: Hofu yatanda Mashariki ya Kati baada ya mashambulizi ya Iran

Guterres jana Jumanne alitoa taarifa fupi akiyataja tu ''mashambulizi ya hivi karibuni huko Mashariki ya Kati" huku akilaani mzozo huo unaozidi kuongezeka. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ataongoza mkutano wa viongozi wa kundi la mataifa saba yenye nguvu kubwa kiuchumi la G7 kujadiliana mzozo huo na kusema Italia itaendelea kuhamasisha suluhu ya kidiplomasia.