TEL AVIV:Israel yamlenga Waziri Mkuu wa Palestina
23 Mei 2007Matangazo
Israel imesema kuwa Waziri Mkuu wa Palestina kutoka kundi la Hamas Ismail Haniya huenda akawa mmoja wa walengwa katika mashambulizi ya anga watakayofanya.
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Israel Ephraim Sneh akizungumza katika radio ya taifa ya nchi hiyo, amesema kuwa hakuna kamanda au kiongozi yoyote wa chama cha Hamas mwenye kinga dhidi ya mashambulizi ya Israel.
Hatua hiyo ya Israel inatokana na shambulizi la roketi lililorushwa na wanamgambo wa kipalestina kutokea Gaza ambalo lilipelekea kifo cha mwanamke mmoja wa Kisrael na wengine wawili kujeruhiwa.
Hapo jana ndege za Israel zilishambulia katikati ya Gaza zikilenga nyumba za viongozi wa Hamas, ambapo mamlaka ya wapalestina imesema kuwa watu saba walijeruhiwa.