1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Telegram yamkamatisha mtuhumiwa ugaidi Ujerumani

2 Januari 2017

Mtu mmoja amekamatwa baada ya mawasiliano yake kupitia mtandao wa Telegram kuonesha aliwasiliana na kundi la kigaidi lijiitalo Dola la Kiislamu akiomba dola 190,000 kununulia malori la kufanyia mashambulizi.

https://p.dw.com/p/2V9kp
Smartphone - Islamischer Staat Anzeige für Sex-Sklavin
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Alleruzzo

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 38 na aliyeingia Ujerumani mwaka 2014 kama muomba hifadhi, alikamatwa katika mji wa Saarbrucken ulio mpakani na Ufaransa, baada ya mpasha taarifa wa polisi kuchati naye kwa mtandao wa Telegram.

Mshukiwa huyo amekiri kuwasiliana na wapiganaji wa IS, lakini amekanusha mashitaka ya kupanga mashambulizi ya kigaidi.

Waendesha mashitaka wanamtuhumu kwa kuwasiliana na mtu ndani ya Syria "ambaye alijuwa kuwa anayo nafasi ya kupata fedha za IS kwa ajili ya kufadhili ugaidi" mwezi uliopita kupitia ujumbe wa Telegram. 

Tayari mshukiwa huyo alishaomba euro 180,000 ambazo angeliweza kuzitumia kununua na kuyatengeneza magari aliyodhamiria kuyajaza mabomu kabla ya kuyaendesha kwenye mikusanyiko ya watu, wanasema maafisa wa upelelezi.