Janga
Tetemeko kubwa la ardhi laua karibu watu 100 Tibet
7 Januari 2025Matangazo
Tetemeko hilo la ardhi la ukubwa wa 7.1 katika kipimo cha richta lilipiga eneo la takriban kilomita 10 na kusababisha vifo na kuporomosha majumba mengi kwenye eneo la kaunti ya Dingri kaskazini mwa mlima Everest na kiasi kilomita 400 kutoka kaskazini mwa mji mkuu wa Tibet Lhasa.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa karibu nyuma 1000 zimeharibiwa na watu 130 wamejeruhiwa, mbali na vifo, vikinukuu makao makuu ya msaada wa tetemeko ya Tibet.
Soma pia: Watoto 68,000 Nepal wahitaji msaada
Jeshi la China limepeleka droni kufanya uchunguzi wa hali ilivyo kwenye eneo hilo. Shughuli za uokoaji zinaendelea na wakaazi wanaondolewa kwenye eneo hilo ili kuzuia athari za uwezekano wa matetemeko mengine madogo yanayofuatia.