1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Idadi ya waliokufa kwa tetemeko la ardhi Ufilipino yafikia 7

18 Novemba 2023

Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lenye nguvu kusini mwa Ufilipino imeongezeka na kufikia watu saba.

https://p.dw.com/p/4Z82t
Tetemeko la ardhi la Ufilipino
Sehemu ya madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi nchini UfilipinoPicha: GenSan City Police Office/Xinhua/picture alliance

Juhudi za uokoaji pia zinaendelea kuwatafuta watu wawili wanaohofiwa kufukiwa kufuatia maporomoko ya ardhi. Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 6.7 lililolikumba eneo la Mindanao mchana wa jana Ijumaa, lilisababisha sehemu ya paa la duka moja kubwa kuporomoka, likisababisha kukatika kwa umeme na watu kukimbilia mitaani. Kulingana na polisi, vifusi vya duka hilo katika mji wa General Santos vilipelekea kifo cha mwanamke mmoja. Waokoaji wanasema tetemeko hilo lilisababisha uharibifu wa nyumba 60 katika mikoa minne pamoja na barabara na madaraja 32 katika eneo hilo.