Timu za Afrika kushuka dimbani kwa mechi za AFCON
7 Septemba 2018Licha ya kuwa na matokeo duni katika nyadhifa zake tatu za ukufunzi, Seedorf mwenye umri wa miaka 42 amepewa mkataba wa miaka minne na mabingwa wa Afrika Cameroon: Mechi yake ya kwanza na timu ya Simba wa Nyika itakuwa ugenini dhidi ya Visiwa vya Komoro katika Kundi B Jumamosi.
Cameroon wana tikiti kama wenyeji ya kucheza katika dimba hilo la Kombe la Mataifa ya Afrika 2019 lililotanuliwa hadi timu 24, lakini wakajumuishwa kwenye mashindano ya kufuzu ili kuwapa mazoezi ya kutosha.
Misri ilimteua Mmexico Javier Aguiire, mwenye umri wa miaka 59 ambaye aliifunza timu ya taifa lake na Japan pamoja na vilabu kadhaa vya Uhispania, ikiwemo Atletico Madrid.
Anachukua nafasi ya Hector Cuper, muargentina ambaye hakuongezewa mkataba baada ya Mapharao hao kufanya vibaya katika Kombe la Dunai kwa kushindwa mechi zote tatu za hatua ya makundi.
Kazi yake ya kwanza ni nyumbani dhidi ya Niger na ni kama suala kuu litakuwa tu ni mabao mangapi ambayo nyota Mohammed Salah atatia kimyani.
Wakati makocha wengi wapya sio Waafrika, maafisa wa Tanzania waliochoka na ukosefu wa matokeo mazuri kutoka kwa makocha wa Ulaya, wameamua kumpa mikoba ya kazi nyota wa Nigeria Emmanuel Amunike. Tanzania inatumai kuwa atawaondoa katika kiwango cha chini na angalau kuwafikisha katika kiwango cha Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38. Taifa Stars watakuwa Uganda kuangushana na wenyeji Uganda Cranes
Mwandishi: Bruce Amani/afp
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman