1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu za Bundesliga zaendesha kampeni ya Ujumuisho wa jamii

14 Septemba 2012

Ligi ya soka ya Ujerumani, Bundesliga, yaingia katika mchezo wa tatu wiki hii.Timu 18 za Bundesliga zitacheza bila ya nembo za wadhamini wa kibiashara, kwa kufanya kampeni ya kuvumiliana na ujumuisho katika jamii.

https://p.dw.com/p/169RY
Bundeskanzlerin Angela Merkel (r, CDU) und der Präsident des FC Bayern München, Uli Hoeneß präsentieren am Donnerstag (13.09.2012) im Bundeskanzleramt in Berlin Trikots und Ball mit der Aufschrift "Geh deinen Weg". Alle Bundesliga-Vereine werden am 3. Spieltag auf ihre übliche Trikotwerbung verzichten und die Spieler mit speziellen Shirts aufs Feld schicken: Mit der Aufschrift «Geh deinen Weg» wollen die Vereine das gleichnamige Projekt der Deutschlandstiftung Integration unterstützen. Foto: Kay Nietfeld dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++ pixel
Angela Merkel rais wa bayern Munich Uli HöneßPicha: picture-alliance/dpa

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezitaka timu zote 18 zinazoshiriki ligi ya Ujerumani , Bundesliga , kuhimiza zaidi kuvumiliana pamoja na ujumuisho katika jamii kwa wahamiaji nchini Ujerumani na kutotumia nembo ya wafadhili wa vilabu hivyo kwa wiki hii.

Club hizo zitatoa sehemu ya pato lao la udhamini huo na kauli mbiu ya kampeni hiyo inasema , Geh Deinen Weg, ikiwa na maana ya "shika njia yako", ama "fuata njia yako". Kansela Angela Merkel atashiriki katika kampeni hiyo kwa kuhudhuria mchezo wa ligi hii leo , ambapo atakuwa mjini Dortmund kushuhudia mchezo kati ya Borussia Dortmund na Bayer Leverkusen.

Dortmund head happy coach Juergen Klopp reacts during the German first division Bundesliga soccer match between Borussia Dortmund an VfL Wolfsburg in Dortmund, Germany, Saturday, Nov. 5, 2011. (Foto:Martin Meissner/AP/dapd) - NO MOBILE USE UNTIL 2 HOURS AFTER THE MATCH, WEBSITE USERS ARE OBLIGED TO COMPLY WITH DFL-RESTRICTIONS, SEE INSTRUCTIONS FOR DETAILS -
Kocha wa Borussia Dortmund Jürgen KloppPicha: dapd

Kwa upande wa michezo yenyewe, baadhi ya timu za bundesliga zimekumbana na hali ngumu. Timu nne hadi sasa zimeambulia patupu. SV Hamburg, Augsburg, Hoffenheim na Stuttgart bado zinasubiri kupata point za kwanza msimu huu.

Baada ya kipigo cha mabao 6-1 dhidi ya Bayern Munich, VFB Stuttgart inashikilia mkia katika msimamo wa ligi ya Ujerumani, Bundesliga. Kocha wa VFB Stuttgart , Bruno Labadia, hata hivyo, anasema kuwa atasubiri hadi katika mchezo wa kumi wa Bundesliga , ndipo aweze kusema lolote kuhusu Stuttgart ilivyofanya. Anasema sasa hivi ni mapema mno kusema kuwa Stuttgart inaporomoka.

"Tunapaswa kufungamanisha , pale tulipokuwa katika mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Wolfsburg. Kwa kulinganisha na matokeo mengine, nafikiri dhidi ya Wolfsburg tulicheza vizuri sana , na tulishindwa kwa bahati mbaya sana.

Lakini iwapo tutaendelea kucheza aina hii ya soka , tutaweza haraka kupata point bila shaka katika ligi hii. Kwangu mimi , ni kwamba baada ya michezo kumi ndio naweza kujiuliza mwanzo ulikuwaje."

Stuttgart inatiana kifuani na Fortuna Düsseldorf , Hoffenheim inawania point yake ya kwanza msimu huu kwa kupambana na SC Freiburg. Hamburg SV ikiwa na mchezaji kutoka Uholanzi ambaye amewasili hivi karibuni kutoka Totenham Hort Spurs ya Uingereza , ina miadi na Eintracht Frankfurt, ambayo mbali ya kupanda daraja imekuwa hadi sasa timu iliyofanya vizuri zaidi baada ya kupata ushindi katika michezo yake miwili ya mwanzo.

viongozi wa ligi hiyo hadi sasa, Bayern Munich , inajaribu kuiweka mbali Borussia Dortmund kwa kupambana na Mainz 05. Na Borussia Dortmund inacheza nyumbani na Bayer Leverkusen.

Na huko nchini Tanzania, ligi kuu ya nchi hiyo imeanza rasmi hii leo Jumamosi, ambapo itafanyika michezo sita. Mabingwa watetezi Simba wamepambana na African Lyon mjini Dar Es Salaam, Yanga imepambana na Tanzania Prisons, na Azam inakwaana na Kagera Sugar.

Mwandishi: Sekione Kitojo / ZR /

Mhariri : Othman Miraji.