1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Tinubu akaribia kupata ushindi wa uchaguzi nchini Nigeria

28 Februari 2023

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa Nigeria yanaonesha Bola Tinubu kutoka chama tawala anakaribia kupata ushindi. Hayo ni kwa mujibu wa hesabu za shirika la habari la Reuters katika majimbo 31 kati ya 36 pamoja na mji mkuu

https://p.dw.com/p/4O57q
Nigeria | Nach den Wahlen | Mahmood Yakubu
Picha: Olukayode Jaiyeola/NurPhoto/picture alliance

Huku yakiwa yamesalia majimbo matano pekee kumtangaza mshindi, Tinubu wa chama cha All Progressives Congress, APC, anaongoza na karibu asilimia 35 au milioni 7.5 ya kura halali zilizohesabiwa, kumaanisha kuwa kuna uwezakano mkubwa atatangazwa mshindi leo wa uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa rais anayeondoka Muhammadu Buhari pia wa APC.

Atiku Abubakar wa chama kikuu cha upinzani, Peoples Democratic, PDP, anafuata akiwa na asilimia 29 au karibu milioni 6.2 ya kura halali. Peter Obi wa chama kidogo cha Labour ana asilimia 25 au karibu milioni 5.2. Vyama viwili vikuu vya upinzani PDP, na Labour vimetoa wito wa kufutwa uchaguzi huo, vikidai kuwepo uchakachuaji wa matokeo na kutaka uchaguzi mpya uitishwe.