Tofauti zaibuka katika mkutano wa COP29
13 Novemba 2024Tofauti hizo zimejitokeza kwenye mkutano wao unaoongozwa na Umoja wa Mataifa unaoendelea nchini Azerbaijan.
Hayo yanajiri wakati ambapo ripoti mpya inatoa wito kwa dunia kuitaka ifikie lengo la kuondosha kabisa hewa ya kaboni mapema zaidi kuliko ilivyopangwa.
Ripoti hiyo imetolewa kwa viongozi hao wanaokutana nchini Azerbaijan kwa ajili ya mkutano wa COP29, kujadili lengo la kufikia makubaliano juu ya kuongeza fedha ili kuyasaidia mataifa yanayoendelea kukabiliana na majanga ya hali ya hewa na pia kugharamia mchakato wa kuhamia kwenye nishati safi.
Kulingana na ripoti hiyo, ili kufikia lengo kuu la makubaliano ya Paris la kupunguza joto hadi nyuzi joto 1.5, dunia sasa ingehitaji kufikia hatua ya kuondosha kabisa, hewa chafu hadi ifikapo mwishoni mwa miaka ya 2030 badala ya miaka ya 2050
Nchi zinazoendelea zinazitaka nchi tajiri zitenge kiasi cha dola trilioni 1.3 kila mwaka kwa ajili ya kuzisaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.