1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Toni Kroos mwanasoka bora wa mwaka wa Ujerumani

4 Agosti 2024

Aliyekuwa kiungo wa timu ya taifa ya UjerumaniToni Kroos kwa mara nyingine tena amepigiwa kura kuwa mwanasoka bora wa kiume wa mwaka kwa Ujerumani, ikiwa ni muda mfupi baada ya kustaafu soka.

https://p.dw.com/p/4j5tu
Robo fainali | Uhispania - Ujerumani | Toni Kroos
Mchezaji Toni Kroos anaonekana mwenye huzuni baada ya Julai 5, 2024 Picha: Kai Pfaffenbach/REUTERS

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, aliyecheza mechi yake ya mwisho ya kulipwa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya 2024, katika hatua ya robo fainali dhidi ya Uhispania mwezi uliipita, katikakuraya maoni ya jarida la michezo la Kicker ameibuka mshindi, mbele ya Florian Wirtz wa Leverkusen na Granit Xhaka.

Mwenyewe amesema matokeo hayo ni uthibitisho mzuri na utambuzi mkubwa wa kile alichokifanikisha kwa mwaka uliopita. Mwaka 2018 Kroos pia alichaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka.