1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trudeau alaani shambulizi dhidi ya jamii ya Waislamu Canada

9 Juni 2021

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau amelaani mauaji ya watu wa familia ya Kiislamu yaliyofanywa na dereva wa lori katika shambulizi lililotajwa kuwa la kigaidi lililochochewa na chuki ya kidini

https://p.dw.com/p/3ud8R
Kanada Trauer um die Opfer des Anschlags auf eine muslimische Familie
Picha: Nathan Denette/REUTERS

Trudeau amesema kwenye hotuba yake mbele ya bunge kwamba mauaji hayo hayakua ni ajali, bali shambulizi la kigaidi lililochochewa na chuki katikati ya moja ya jamii za nchini humo.

'Tunaweza kusema nini wakati wapendwa wa familia nyingine wakiwa wamechukuliwa, wakati mtoto yuko hospitalini, wakati jamii inaomboleza? Kwa hivyo ninachoweza kusema ni hiki: Kwa kila mtu anayehuzunika, aliye na hasira, anayeogopa, majirani zako wanasimama na wewe. Jamii yako inasimama nawe. Hatutaruhusu chuki itugawanye,'' alisema Trudeau.

soma zaidi: Muuaji wa Canada alikuwa na chuki dhidi ya Waislamu - Polisi

Waziri Mkuu Justin Trudeau aliyaita mashambulizi hayo kuwa ni "habari za kuogofya", akiongeza kwamba chuki dhidi ya Waislamu hazina nafasi kwenye jamii ya Canada. 

Shambulizi hilo lilitokea Jumapili wakati lori lilipowakanyaga na kuwaua watu wanne wa familia moja katika mji wa London, kwenye jimbo la Ontario.

Mtoto mmoja aliyenusurika katika shambulizi hilo bado anatibiwa