Trump apiga marufuku mahusiano na wamiliki wa Tik Tok
7 Agosti 2020Hatua hiyo hata hivyo haijajulikana iwapo rais wa Marekani ana mamlaka ya kisheria kupiga marufuku app hiyo nchini Marekani.
Amri hizo mbili za utendaji, moja kwa kila app, inaanza kutumika katika muda wa siku 45 zijazo. Zinamtaka waziri wa biashara kufafanua utendaji wa marufuku hizo kwa wakati huo. Wakati maelezo ya amri hizo hayaeleweki, baadhi ya wataalamu wamesema inaonekana zina lenga kuzuwia app hizo maarufu kuwekwa katika app inayohifadhi app kama hizo katika Apple na Google, hali ambayo inaweza kuziondoa kabisa katika usambazaji wa app hizo nchini Marekani.
"Haya ni matumizi yasiyo kifani ya mamlaka ya rais," Mchambuzi wa kundi la Eurasia Paul Triolo alisema katika barua pepe. Kw uchache amesema, amri hiyo inaonekana, kuweka marufuku juu ya uwezo wa hifadhi ya app nchini Marekani inayoendeshwa na kampuni ya Apple na Google na kujumuisha app ya simu za mkononi baada ya siku 45.
Triolo alisema amri hiyo huenda ikakumbana na vipingamizi vya kisheria na kuonya kuwa China huenda , ikachukua hatua kali, takriban kwa matamshi makali.
Sheria ya dharura
Amri ya Trump inaelezea kuhusu mamlaka ya sheria, ya sheria ya kimataifa ya dharura ya uwezo wa kiuchumi na sheria ya dharura ya taifa.
Utawala wa Trump imekuwa ikipambana na kitisho kutoka China , na wabunge wote wa chama cha Republican na Democrats pia wameonesha wasi wasi juu ya Tik Tok, ikiwa ni pamoja na uchujaji taarifa, kampeni zinazotoa taarifa zisizo sahihi, usalama wa data za watumiaji na faragha kwa watoto. Lakini utawala huo haujatoa ushahidi mahsusi kwamba Tik Tok imetoa data za watuamiaji nchini Marekani kwa serikali ya China. Badala yake , maafisa wanaelekeza katika kitisho cha kufikirika ambacho kinatokana na uwezo wa serikali ya China kudai ushirikiano kutoka kwa makampuni ya China.
Mapewa wiki hii, Trump alitoa kitisho cha muda wa mwisho wa Septemba 15 kufunga shughuli za Tik Tok hadi pale kampuni ya Microsoft ama kampuni nyingine itakapoinunua kampuni hiyo. Siku ya Jumatano , waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alitangaza upanuzi wa mapambano ya Marekani dhidi ya teknolojia ya China ikiwa ni pamoja na kuzipiga marufuku app za China katika hifadhi ya makampuni ya Marekani ya app hizo, akielezea madai ya kitisho cha usalama na kuzitaja kwa majina Tik Tok na WeChat.