Marekani: Trump ashinda muhula wa pili wa kihistoria
6 Novemba 2024Trump amempiku Mdemocrat makamu wa rais Kamala Harris katika kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu ya White House.
Televisheni za Marekani zimemtangaza mshindi baada ya matokeo kuonyesha kuwa amepata zaidi ya kura 270 za wajumbe wa kamati maalum ya uchaguzi anazohitaji.
Alimbwaga Harris katika majimbo yenye ushawishi yakiwemo Pennsylvania na Wisconsin. Akiwahutubia wafuasi wake mapema leo, Trump alisema ni wakati sasa wa kuliponya taifa.
Soma pia:Trump ajitangaza mshindi wa urais Marekani
Viongozi wa Ulaya wakiwemo wa Ufaransa, Ujerumani na Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa waliotuma salamu za mapema za kumpongeza Trump wakiahidi kufanya kazi pamoja.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte pia wamempongeza.
Hakuna salamu zilizotoka Moscow mpaka sasa, ambako msemaji wa Rais Vladmir Putin, Dmitry Peskov, ametangaza kuwa uhusiano wa Urusi na Marekani umefikia kiwango cha chini mno katika historia. China pia imejiuzuwia mpaka sasa kutoa salaam za pongezi kwa Trump.