1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump asusia mdahalo wa kwanza wagombea urais wa Republican

24 Agosti 2023

Wanasiasa wanane wanaowania tiketi ya kugombea urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani wamechuana usiku wa kuamkia leo katika mdahalo wa kwanza kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024.

https://p.dw.com/p/4VWFo
USA Donald Trump
Donald Trump anaongoza kura za maoni za kuwania tiketi ya Republican uchaguzi wa 2024Picha: ROBYN BECK/AFP/Getty Images

Mdahalo huo uliodumu kwa muda wa saa mbili na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Fox News, umegusia masuala tete yanayotarajiwa kuwa ajenda ya uchaguzi ujao ikiwemo uhalifu, utoaji mimba na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Miongoni mwa walioshiriki ni Gavana wa Jimbo la Florida, Ron Desantis, anayepewa nafasi ya kutoa ushindani kwa rais wa zamani, Donald Trump, anayewania kupeperusha bendera ya chama cha Republican na ambaye hata hivyo hakushiriki mdahalo huo.

Wengine ni makamu wa rais wa zamani chini ya Trump, Mike Pence, na balozi wa zamani wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley.