Trump kuiwekea vikwazo Urusi ikikataa mazungumzo ya mani
22 Januari 2025Matangazo
Hata hivyo, hakutoa ufafanuzi juu ya aina ya vikwazo vipya, ingawa tayari Marekani imeiwekea Urusi vikwazo vikali kufuatia uvamizi wake wa Februari 2022.
Trump pia alidokeza kwamba serikali yakeinatafakari suala la kutuma silaha kwa Ukraine, akiongeza maoni yake kwamba Umoja wa Ulaya unapaswa kufanya mengi zaidi kuiunga mkono Ukraine.
Soma pia: Trump asema atakutana 'haraka sana' na Putin.
Alisema wako katika mawasiliano na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, na wanatarajia kuzungumza na Putin hivi karibuni.
Vilevile, Trump alieleza kuwa alimhimiza Rais wa China, Xi Jinping, kutumia ushawishi wake kumaliza vita hivyo, akibainisha kuwa licha ya China kuwa na nguvu kubwa, Xi hajaonyesha juhudi za kutosha kusitisha mgogoro huo.