Trump kukamatwa Jumanne
1 Aprili 2023Haya ni kwa mujibu wa maafisa wa mahakama, hili likiwa tangazo la kihistoria kwa rais wa zamani nchini humo kufikishwa mahakamani.
Wakati mahakama ya Manhattan ilipothibitisha muda huo hapo jana, barabara nje ya mahakama hiyo zilikuwa zimetulia baada ya maandamano yaliyoshuhudiwa mapema wiki iliyopita lakini umati mkubwa wa wanahabari na polisi ulishuhudiwa.
Soma zaidi:Trump kushtakiwa kufuatia malipo kwa Stormy Daniels
Katika mahojiano ya televisheni hapo jana, wakili wa Trump, Joseph Tacopina, alisema atapinga vikali uhalali wa kisheria wa uamuzi wa jopo la mahakama hiyo wa kumshtaki rasmi Trump.
Kupitia mitandao ya kijamii, Trump ameeleeza hasira yake na kulalamika kuwa jaji anayetarajiwa kushughulikia kesi hiyo, Juan Manuel Merchan, anamchukia.