1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump na Harris kuendelea na kampeni za mwisho mwisho

Sylvia Mwehozi
27 Oktoba 2024

Wagombea urais nchini Marekani leo wanaendelea na kampeni ikiwa imesalia zaidi ya wiki moja kabla ya uchaguzi wa Novemba 5.

https://p.dw.com/p/4mHoH
Wagombea urais nchini Marekani Donald Trump na Kamala Harris
Wagombea urais nchini Marekani Donald Trump na Kamala HarrisPicha: Jim WATSON and Brendan Smialowski/AFP

Wagombea urais nchini Marekani leo wanaendelea na kampeni ikiwa imesalia zaidi ya wiki moja kabla ya uchaguzi wa Novemba 5. Mgombea wa Republican Donald Trump atapiga kampeni katika viunga vya bustani maarufu ya Madison Square jijini New York leo, wakati mpinzani wake Kamala Harris akipita kitongoji kwa kitongoji huko Philadelphia. Mkutano wa Trump hapo Madison Square utahudhuriwa na wafuasi 20,000 na watu maarufu akiwemo bilionea Elon Musk ambaye amejitosa kumpigia kampeni.

Harris amepanga kufanya kampeni katika jiji kubwa linalohitaji ushindi la Pennsylvania. Wagombea wote wawili wanapiga kampeni za mwisho mwisho kwa wapiga katika moja ya uchaguzi uliojaa migawanyiko nchini Marekani. Uchunguzi wa kura za maoni unaonyesha kinyang'anyiro kikali baina ya Trump na Harris kuelekea kura ya Novemba 5.