Rais Felix Tshisekedi amefanya mageuzi makubwa katika jeshi la DRC na kuwateua maafisa wa karibu naye kuchukuwa nyadhifa muhimu za jeshi. Luteni Jenerali Christian Tsiwewe Songesha ameteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Kongo akichukuwa nafasi ya Celestin Mbala. Tatu Karema amezungumza na Saleh Mwanamilongo kuhusu umuhimu wa mabadiliko hayo.