Tshisekedi ateua kamanda mpya operesheni za kijeshi
6 Septemba 2023Hayo yanajiri wakati huu ambapo kesi ya wanajeshi 6 waliohusika katika ukandamizaji mbaya dhidi ya maandamano ya raia, ikianza kusikilizwa tangu Jumanne na mahakama kuu ya kijeshi mjini Goma. Washtakiwa hao ni maafisa wawili wa jeshi la FARDC, kanali Mike Mikombe na Luteni kanali Donatien Bawili ambao serikali ilitangaza kuwakamata pamoja na askari wa nne wa vyeo vya chini.
Hata hivyo, mashirika ya kiraia katika mji huu wa Goma yanayopoteza matumaini kwa vyombo vya usalama, yameomba kuondolewa mara moja kwa uongozi huo wakijeshi wanaoutuhumu kuhusika na visa vya uhalifudhidi ya raia hasa wakati huu ambako zaidi ya watu 150 ambao ni waumini wa dhehebu la kizalendo wanaendelea kuzuiliwa korokoroni, Mario Ngavo ni afisa mkuu wa asasi za kiraia mjini Goma .
Wakati huo huo, serikali imemtangaza Jenerali Chaligonza Nduru kuwa kaimu gavana wa kijeshi na kamanda wa operesheni za kijeshi zinazoendelea kurejesha usalama mkoani humo, akichukuwa nafasi ya Lt.Constant NDIMA ambaye amerejesha mjini Kinshasa kwa mahojiano. Aidha, raia hao wanaoendelea kuwakumbuka wapendwa wao waliofariki katika maandamano hayo kwakupigwa risasi, waelezea hisia zao.
Hatua hiyo ya serikali,imejiri baada ya ujumbe wa mawaziri kutoka kinshasa kumaliza ziara yao hapa mjini Goma ambako waliahidi kutoa mwanga juu ya tukio hilo la Agosti 30.