Tutabakia ICC kama Marekani nayo itajiunga - Namibia
2 Desemba 2016Matangazo
Akizungumza na shirika la habari la Uingereza jijini London, Rais Hage Geingob wa Namibia amesema anaamini ICC inawalenga Waafrika pekee, msimamo ambao pia unachukuliwa na mataifa mengine kadhaa ya bara hilo.
Mnamo mwezi Machi, Namibia ilitangaza kwamba itajiondoa mahakama hiyo ya mjini The Hague, ambayo ina mamlaka ya kisheria kuwashtaki watu binafasi kwa kuhusika na mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.
Rais Geingob ambaye alichaguliwa kuingia madarakani mwezi Novemba mwaka 2014 ameongeza kwamba ikiwa Marekani itajiunga na ICC, basi na Namibia nayo itaendelea kuwa mwanachama.
Marekani kwa sasa sio mwanachama wa Mkataba wa Roma unaoisimamia mahakama hiyo.