BoBs Wettbewerb
15 Februari 2012Kulinganisha na mwaka jana ambapo mengi yalihusiana na hali ya mageuzi katika nchi za kiarabu, mwaka huu uzito mwingi uko katika nyanja za utamaduni na elimu. Katika upande wa," Tuzo maalumu ya masuala ya Elimu na Utamaduni“ patatafutwa blogu bora za kuelimisha na mapendekezo ya kushajiisha elimu kutoka lugha zote 11.
Utamaduni, elimu na wajibu wa vyombo vya habari pia ni mada kuu katika jukwaa la vyombo vya habari vya kimataifa ambalo litafanyika mjini Bonn kuanzia tarehe 25 hadi 27 Juni.
Kuimarisha uhuru wa kutoa maoni
Zingatio hasa pia mwaka huu ni tuzo ya tovuti ambazo zinaunga mkono uhuru wa kutoa maoni kwa njia mtandao. Wagombeaji wanaweza pia kushughulikia masuala mengi, kama vile blogu zenye kutoa taarifa mbadala katika nchi zisizo na vyombo huru vya habari au mambo muhimu ambayo husaidia kujenga jumuiya za kiraia. Blogu itakayokuwa na nafasi ya kushinda bila shaka ni ile iliyofanya kampeni ya kuunga mkono demokrasia, uhuru na haki za binadamu.
Tuzo katika orodha ya “wanahabari wasio na mipaka” itatolewa kwa ushirikiano na Shirika la wanahabari wasio na mipaka(RSF). Katika orodha hii ni zile blogu na tovuti zilijojishuhulisha kwa undani kuhusu masuala ya uhuru wa kutoa maoni.
Uwezekano wa washiriki tafauti:
Kutokana na tuzo hili, kutakuweko na tovuti ya mashindano haya kwa lugha zote 11 Kiarabu, Kibengali, Kichina, Kijerumani, Kiingereza, Kifaransa, Kiindonesia, Kireno, kirusi na kihispania.
Katika mashindano haya, kila mtumiaji mtandao anaombwa kutoa mapendekezo yake. Kisha mapendekezo hayo hukusanywa kupitia njia rahisi katika tovuti ya shindano. Zaidi ya hayo, kila mtumizi hungia kupitia mtandao wa Facebook au Twitter na kilicho kipya mwaka huu ni ule mtandao wa lugha ya Kirusi wa Vcontact, Twitter ya Kichina Sina Weibo au kupitia OpenID
Majaji wa kimataifa kuwachagua washindi
Kundi la majaji wa waliotoka nchi mbali mbali limeundwa kutokana na wanaharakati maarufu wa mitandao, wanablogu na wataalam wa internet kutoka maeneo ya lugha 11 zinazotumiwa katika shindano hili. Jaji kutoka Ujerumani mwaka huu ni Patricia Cammarata maarufu kwa jina la “dasnuf” ambaye anaendeleza blogu yake kwa takribani miaka minane iliyopita
Majaji wengine ni mwanablogu na mwanahabari maarufu wa kirusi Alexander Plushev, mwanaharakati na mpiga picha wa Kibengali Shahidul Alam pamoja na Isaac Mao wa China ambaye ni mmoja wa waandalizi wa kongamano la wanablogu wa Kichina.
Baada watumiaji wa mtandao wa internet kupiga kura kumchagua mshindi, hatimae majaji watakutana mwanzoni wa mwezi Mei kumteua mshindi mjini Berlin. Mashindano haya yatamalizika kwa sherehe ambapo majaji watatoa tuzo kwa mshindi huyo tarehe 26 Juni mbele ya kongamano la jukwaa la vyombo vya habari vya kimataifa la Deutsche Welle mjini Bonn.
Mwandishi: Petra Füchsel / Tafsiri: Susan Kiungu
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman