UAE yakana kubainika idadi kubwa ya silaha Sudan
14 Agosti 2023Matangazo
Umoja wa falme za kiarabu umesema haugemei upande wowote katika mgogoro wa Sudan. Waangalizi wamesema pande zote mbili zilizoko vitani nchini Sudan,jeshi la serikali likiongozwa na AbdelFattah el Burhani na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdani Daglo anayeongoza kikosi cha wanamgambo cha RSF wanaongozwa na mataifa ya kigeni huku Misri ikiwa upande wa Burhani na Umoja wa Falme za kiarabu ukiegemea kambi ya Daglo.Hata hivyo jana Jumapili mkurugenzi wa mawasiliano katika wizara ya mambo ya nje ya UAE Afra Al Hameli amesema nchi yake haijawahi kupeleka silaha kwa upande wowote katika vita vya Sudan tangu ulipozuka mgogoro huo.